Tasnifu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The printable version is no longer supported and may have rendering errors. Please update your browser bookmarks and please use the default browser print function instead.

Tasnifu (Kiingereza thesis, dissertation) [1] ni maandiko ya kitaaluma yanayochanganua mada maalumu kwa ajili ya kupata shahada ya juu.

Hutolewa pale ambapo msomi analenga digrii ya kitaaluma akiwasilisha utafiti na matokeo yake. [2]

Katika miktadha mingine, neno "tasnifu" hutumiwa pia kwa kazi kubwa ya kimaandishi iliyo sehemu ya shahada ya awali au ya uzamili, lakini kwa kawaida hutumiwa kwa uzamivu.[3]

Ugumu au ubora wa utafiti unaohitajika kwa tasnifu inaweza kutofautiana na nchi, chuo kikuu, au somo.

Marejeo

  1. Nieves-Whitmore, Kaeli. "Subject Guides: Citation Help: Dissertations & Theses". guides.lib.uiowa.edu (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 15 February 2021.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. International Standard ISO 7144: Documentation—Presentation of theses and similar documents, International Organization for Standardization, Geneva, 1986.
  3. Douwe Breimer, Jos Damen et al.: Hora est! On dissertations, Leiden University Library, 2005.

Viungo vya nje