+++ to secure your transactions use the Bitcoin Mixer Service +++

 

Nenda kwa yaliyomo

Amazon (kampuni)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 06:32, 20 Oktoba 2018 na Ndesanjo (majadiliano | michango) (Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ' '''Amazon.com, Inc.''', (inafanya biashara kama Amazon), ni kampuni ya Marekani yenye makao makuu Seattle, Washington, ambayo ilianzishwa na Jeff Bez...')
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)

Amazon.com, Inc., (inafanya biashara kama Amazon), ni kampuni ya Marekani yenye makao makuu Seattle, Washington, ambayo ilianzishwa na Jeff Bezos tarehe 5 Julai 1994. Kampuni hii ndio kampuni kubwa kabisa duniani ya uuazji wa bidhaa kwenye intaneti kutokana na kipimo cha mapato na mtaji wa soko, na ni ya pili baada ya Alibaba Group kwa jumla ya mauzo. Tovuti ya amazon.com ilianza kama duka la vitabu mtandaoni na baadaye ilianza kuuza video, muziki, michezo ya video, nguo, samani, vyakula, vito vya thamani, n.k. Kampuni hiyo pia inamiliki kampuni ya kuchapisha, Amazon Publishing, studio ya filamu na televisheni, Amazon Studios, inatengeneza bidhaa za elektroniki kama vile Kindle, Echo n.k.

Amazon ina maduka ya rejareja katika nchi za Marekani, Uingereza, Ireland, Ufaransa, Canada, Ujerumani, Italia, Hispania, Uholanzi, Australia, Brazili, Japan, China, India, Mexico, Singapore na Uturuki.

Mnamo mwaka 2015, Amazon iliipita kampuni ya Walmart kama kampuni ya uuzaji wa rejaraje yenye thamani kubwa zaidi nchini Marekani. Amazon ni kampuni ya pili ya thamani zaidi duniani (nyuma ya Apple tu), kampuni kubwa ya intaneti kwa mapato duniani, na baada ya Walmart, mwajiri wa pili mkubwa nchini Marekani. Mwaka wa 2017, Amazon ilinunua Whole Foods Market kwa $ 13.4 bilioni. Mnamo Septemba 4, 2018, Amazon ilikuwa na thamani ya dola trilioni 1 za Marekani.

Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos

Bodi ya wakurugenzi

Bodi ya wakurugenzi ni:[1]

Kampuni tanzu

Amazon inamiliki zaidi ya kampuni tanzu 40, ikiwa ni pamoja na Zappos, Shopbop, Diapers.com, Kiva Systems (sasa inaitwa Amazon Robotics), Audible, Goodreads, Teachstreet na IMDb.[2]

A9.com

A9.com ni kampuni inayojihusisha na utafiti na teknolojia tangu 2003. [3]

Amazon Maritime

Amazon Maritime, Inc. ni kampuni inayomiliki meli zinazosafirisha bidhaa za Amazon toka China hadi Marekani.[4]


Amazon Translate

Amazon Translate ni kampuni inayotumia teknolojia ya mashine ya kutafsiri. [5]

Audible.com

Audible.com ni kampuni inayouza bidhaa za burudani ya masikioni kama vile vitabu, vipindi vya televisheni, n.k. Amazon iliinunua kampuni hii kwa dola za Kimarekani milioni $300.[6]


Beijing Century Joyo Courier Services

Brilliance Audio

ComiXology

CreateSpace

Goodreads

Lab126

Shelfari

Twitch

Whole Foods Market

Junglee

Marejeo

  1. "Officers & Directors". Amazon. Iliwekwa mnamo Februari 22, 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Amazon Jobs – Work for a Subsidiary". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Agosti 1, 2014. Iliwekwa mnamo Oktoba 27, 2014. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. McCracken, Harry, "Amazon's A9 Search as We Knew It: Dead!", PC World. September 29, 2006. Retrieved September 6, 2012.
  4. Steele, B., Amazon is now managing its own ocean freight, engadget.com, January 27, 2017, accessed January 29, 2017
  5. Amazon Translation
  6. Sayer, Peter. "Amazon buys Audible for US$300 million", PC World, January 31, 2008. 

External links